Timu ya soka iliyojitambulisha kwa jina la 3pillars ambayo ilkuja chini kwa mechi za kirafiki kucheza na timu za hapa nyumbani ambayo imejitambulisha kwamba imefuzu kucheza ligi kuu ya nigeria ambayo ipo karibuni kuana jana hatimaye imejulikana kwamba hiyo timu haipo katika hatua hizo za ligi na kwani ligi imeshaanza muda mrefu na bado kipindi kidogo imalizike.
Haya yamebainika jana baada ya chombokimoja cha habari chini kuongea mojakwamoja na mwandishi mzoefu wa masuala ya soka kutoka nigeria kuhusu timu hiyo.
Amesema kwamba timu ambayo inajulikana katika ranki au daraja hilo na kanu pillars na sio 3pillars na hakuna timu anayojulikana kwa jina hilo labda katika ngazi za chini kabisa na hata jivyo hana uhakika kama timu hiyo ipo.
Haya yote yamekuja baada ya kuepo zengwe la timu hiyo kudaiwa kuzuiwa kwa kutolipa dena la shilingi million 20 na zaidi katika hotel moja hapa nchini na kutoweza kuondoka hadi hivi sasa.
Swala la kujiuliza je inakuwaje timu inatoka nigeria hawana uwezo wa kulipa hizo fedhana ilihali ligi inaendelea? na vilevile kwa clubu zetu hapa nchini ni lazoma kuwa na uhakika kwani kuna uwezekano mkubwa sana kwamba iyo timu imejikota tu ambao ni vijana wa mitaani ambao hawana timu na kujiita kwa timu yeyote ili wapate fedha tu ukufikiria kwama kuna wanigeria kibao hawana timu na wapo nchini wakizagaa tu.
No comments:
Post a Comment