Saturday, September 7, 2013

GERRARD AMSIFU RICHIE LAMBERT

Kutokana na kusimama kwa ligi mbalimbali duniani na kuipisha michezo ya kimataifa ya kugombania nafasi ya kucheza kombe la dunia mwakani nchini brazil, England jana usiku ilikutana na moldovia katika uwanja wa wembley.

Katika mchezo huo England iiibuka na ushindi wa mabao 4-0 ambapo kaptain wa timu hiyo steven gerrard amemsifia mshambulia wa southermpton richie lambaert baada ya kufunga goli lake la tatu katika timu ya taifa hiyo.

Ilichukuwa dakika za mwanzo tu pale nahodha huyo alipoanza kuiandikia timu yake kwa shuti kali la pembeni na baadae lambert alipiga msumali wa pili kisha danny welberck kupachika bao la tatu na la nne.
Timu hiyo itamkosa mshambuliaji wake danny welbeck  baada ya kuwa na kadi za njano ambazo zitamfanya aikose mechi ya jumanne.

No comments:

Post a Comment