Monday, September 9, 2013

GRAND MALT PREMIUM LEAGUE YAENDELEA, CHUONI YAICHAPA POLISI ZANZIBAR(WAZEE WA TUNISIA)

Ligi kuu ya zanzibar chini ya bia isiyo kuwa na kilevi grand malt imeendelea hii leo katika viwanja viwili vya mao tse tung cha unguja kilicowakutanisha timu ya chuoni na polisi ya zanzibar na gombani pemba kilichowakutanisha timu za kizimkazi na chukwani.

katika uwanja wa mao tse tung timu ya fuoni iliionyesha kazi wazee wa tunisia baada ya kuilamba bao moja bila majibu lililofungwa na goege thomas katika dakika ya 64 ya mchezo na kule pemba timu ya kizimkazi ilishinda bao 4-2 dhidi ya chukwani. magoli ya kizimkazi yalifunwa na ally faki,salim khamis na juma makame aliyefunga bao mbili na yale ya chukwani yalifungwa na mfanyeje juma.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa kuwa kutanisha timuza malindi na mafunzo kwenye uwanja wa mao tse tung.

No comments:

Post a Comment