Monday, September 16, 2013

JULIO: USHIDI DHIDI YA MTIBWA SUGAR NI ZAWADI KWA WANASIMBA WOTE

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya simba jamhuri kihwelo"julio" amesema kwamba ushindi walioupata jumamosi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya mtibwa sugar ya morogoro kwa mabao 2-0 ni zawadi kwa washabiki wote wa timu hiyo.

Juilo ameendelea kusema kwamba ilikuwa ni mechi ngumu kwetu kwa kuwa kila mmoja anawajuwa wapinzani wao walivyo lakini wao walijituma kupitia kwa wachezaji wao hasa baada ya kuingia henri josef na mshambuliaji mombeki.

Amesema kwamba kwa sasa timu ipo kambini na wanafanya mazoezi yao bamba beach huko kigamboni ili kujiandaa na mchezo wao utakaopigwa siku ya jumatano katika uwanja wa taifa dhidi ya mgambo jkt.

No comments:

Post a Comment