Friday, September 6, 2013

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION YAKAMATA COPY FEKI ZA WASANII

Kampuni ya msama prmotion chini ya Alex Msama imeanza kazi ya kutafuta uharamia unaofanywa na watu katika kuiba kazi za wasanii na kunufaika wao na kuwa didimiza wasanii nchini.

Kampuu hiyo ilianza kazi jana ya kukamata kazi feki ambazo huuzwa kwa bei rahisi pamoja na kukamata mtambo unaoendesha shughuli hizo chenye thamani ya shilingi millioni 18.

Kwa mujibu wa mmiliki wa kampinu hiyo Bw Alex msama amesema kwamba wameanza na wataeda kila kona ya ndani ya nchi ili kuweka hali nzuri na kuwatetera wasaanii wetu ambao hufanya kazi kubwa na mwishowe kfaidika wengine.

Vilevile ameongeza kwamba anawaomba watanzana wote tushirikiane katika swala hili na si kuachiwa wao tu kwani mwishowe wasanii wetu wakifanikiwa na kututangaza nje ni fahari ya wananchi wote na si msama promotion, na kusisitiza kwamba si vyema kununua cd kwa shilingi 1000 kwa kuwa ni bei ya chini kwani ni dhulma ambayo tunawafanyia wasanii wetu.

Hii imekuja baada ya miliki wa kampuni hiyo kuchaguliwa katika baraza a sanaa la taifa ambapo alichaguliwa na raisi jakaya kikwete siku mbili zilizopita pamoja na Eric Shigongo wa the publisher. Na kwa kuongezea tu ni kwamba suala hili ni la kuungwa mkono kampuni hii ili kuinua kazi za wasanii wetu nchini.

No comments:

Post a Comment