Monday, September 2, 2013

LUIS NANI ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED

Winga kutoka ureno luis nani hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuitumikia clubu hiyo baada ya kutakiwa na clubu nyingi barani ulaya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka clubuni hapo zinasema kwamba luisi nani amesaini mkataba mpya na anafura kuwa katika clubuni hapo na hakuna mazungumzo yeyote tena kuhusu usajili wa winga huyo.

Awali winga huyo alitakiwa na clubu nyingi kama vile juventas,as monaco na garatasaray  ili kumsajili lakini baada ya kupona majeraha yake yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu na kuhakikishiwa na kocha wake moyes kwamba anaweza kuwa katika kikosi cha kwanza kwani yupo katika mipango yake sas nani aongeza mkataba na timu hiyo na kufunga mazungumzo na timu yeyote inayomuhitaji. 

No comments:

Post a Comment