Saturday, September 21, 2013

TARIBO WEST:"NILIKUWA BORA KULIKO MALDINI AC MILAN"

Beki wa zamani wa kimataifa kutoka Nigeria  the supeman Taribo West amesema kwamba kipindi alipokuwa Ac milan alikuwa bora kuliko mzawa wa timu hiyo Paolo Maldini.

Hayo alisema baada ya kuhojiwa na kituo kimoja cha michezo nchini  Nigeria kuhusiana na maisha yake ya soka kwa ujumla yalikuwaje  mpaka sasa alivyostaafu soka

Tarobo west alisema" kwanza ilikuwa ni wakati mgumu sana kukubalika kwa mchezaji yeyote kutoka barani Afrika kipindi hicho na pia ilikuwa ni kipindi kigumu kumpokonya namba Maldini kwa kuwa yeye ni mzawa na anakubalika na kila shabiki wa soka nchii humo hata akiwa wa timu pinzani".

Aliendelea kwa kusema kutokana na juhudi zangu uwanjani na nikawafanya washabiki wa timu hiyo kunikubali na hata kuthubutu kusema nilikuwa bora kuliko Maldini.

Beki huyo pia amesha wahi kuchezea timu ya taifa ya Nigeria kwa miaka mingi ikiwemo kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2000.

No comments:

Post a Comment