Thursday, September 19, 2013

TFF YATOA SIKU 14 KWA TIMU ZA LIGI KUU NA DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA

Shirikisho la soka nchini tanzania TFF kupitia kwa kamati ya katiba,maadili na hadhi ya wachezaji limetoa siku 14 kwa timu zote za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kupeleka mikataba ya makocha wote wa timu hizo.

 Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati hiyo bwana Alex Mbongolwa amesema kwamba taarifa hiyo ilshatoka kipindi kirefu sasa laini cha kushangaza hadi hivi sasa hakuna timu iliyoleta mikataba ya benchi la ufundi la timu husika

Vilevile ameongeza kuwa kama clubu ikichelewa kuwasilisha mikataba hiyo itatozwa faini na uongeza kwamba hii ni lazima kwa mujibu wa katiba ya TFF kwa kila timu kuwasilisha mikataba ya makocha wao kwani hadi hivi sasa baadhi ya makocha hawana mikataba katika timu zao.

No comments:

Post a Comment