Thursday, October 24, 2013

AKIWA ANASHEREHEKEA MIAKA 26 TANGU KUZALIWA KWAKE LEO, WYNE ROONEY AFURAHIA MAISHA NDANI YA MANCHESTER UNITED CHINI YA KOCHA MPYA MOYES

Baada ya leo kuwa ni siku yake ya kuzaliwa  akiwa anaadhimisha miaka 28 tangu kuzaliwa kwake nyota wa timu ya Manchester United na timu ya taifa ya England Wyne Rooney amesema kwamba anafuraha sana katika maisha yake ya sasa chini ya kocha mpya Moyes.

Nyota huyo tegemezi wa timu ya Man United na timu ya taifa lake amesema  kwamba kwa sasa anafuraha kubwa ndani ya timu hiyo kushinda kipindi cha kocha aliyejiuzulu kuifundisha timu hiyo Sir Alex Ferguson.


Rooney ameongea kwamba kiufundi anafurahi sana kupangwa sehemu ambayo anaimudu akiwa uwanjani na kuongeza kwamba anajisiia vizuri kubaki ndani ya timu hiyo na sasa anamipango mizuri na timu hiyo hasa baada ya kutoanza vizuri msimu huu na kusisitiza kwamba anaimani watafanya vizuri katika michuano mbalimbali msimu huu japokuwa wameanza vibaya.

Awali nyota huyo alisadikika kuondoka clabuni hapo kutokana na kutoridhika kuambiwa yeye ni chaguo la pili
katika kikosi cha kocha aliyepita. Lakini kwa sasa anafuraha hasa baada ya kupata nafasi ya kwanza na kuanza kufurahia maisha mapya na kocha mpya.

Vilevile aliulizwa kuhusiana na kitabu kilichooka cha kocha wake wa zamani kwani na yeye amezungumziwa kutokana na kutaka kuondoka kipimdi cha Ferguson na kusema kwamba"Sija kutana na Ferguson tangu astaafu kufundisha timu hii lakini mambo ya kitabu  hayanihusu hata kidogo kwani yasha pita na sasa tunaangalia mengine."

No comments:

Post a Comment