Sunday, October 13, 2013

ROONEY AKATAA KUFUNGUA MAZUNGUMZO YA KUIMARISHA MKATABA WAKE MANCHESTER UNITED

Mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Uingereza na clabu ya Manchester united wyne rooney amekataa kufungua mazungumzo ili kuongeza mkataba.

Nyota huyo amekataa kufungua mazungumzo ya kuongeza mkataba na timu yake hiyo yenye maskani yake jijini manchester.

Hii imekuja baada ya nyota huyo kuimarika katika kiwango chake kwa sasa a kuthibitisha kwamba atabaki clabuni hapo baada ya kumalizika dirisha  la usajili lililopita ambapo alitakiwa na vilabu vingi ikiwemo matajiri wa london chelsea.

Rooney amekataa kufungua mazungumzo na timu hiyo na kuleta hali ya sitofahamu ndani ya timu hiyo na kuanza kuthibitika muda wowote nyote huyo ataondoka licha ya kusema hataondoka.

Mkataba wa Wyne Rooney na the red devils unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu wa 2014-2015 na ndio maana uongozi wa timu hiyo unataka kumuongeza mkataba.

No comments:

Post a Comment