Kiungo wa kimataifa wa uingereza na clabu ya Arsenal Jack Wilshere amekanusha kusema kwamba alikitaka chama cha soka cha uingereza kumshawishi nyota chipukizi wa timu ya manchester united Adnan Januzaj ili aichezee timu ya taifa hilo.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vilichapisha habari hiyo baada ya kuona mjadala wake na washabiki wa nyota kuhusiana wachezaji wa timu ya taifa ya uingereza ambao sio wazawa katika mtandao wa twitter.
Awali jumapili iliopita kocha wa timu ya manchester united alibainisha kwa kusema kwamba chama cha soka nchini humo kinataka kuzungumza na Jauzaj kuhusiana na swala la kuichezea timu ya taifa hilo, ambapo kutokana na kauli hiyo Wilshere alisema kupitia Twitter kwamba Januzaj halazimishwi kuchezea timu hiyo kwa kuwa yeye sio muingereza.
Lakini kwa upande mwingine waandisha walielewa kwamba Wilshere ameiomba FA kumshawishi Januzaj.
Wilshere alisema kwamba ameshangaa wandishi hao kuchapisha habari hiyo kwani itapelekea kwake kuonekana mtu wa ajabu.
Janzaj hadi sasa amefikisha miaka 19 na bado hajasema taifa gani atalitumukia katika michezo ya kimataifa na bado hajachezea timu yeyote ya taifa na ndio maana chama cha soka cha uingerteza kinataka kufungua mazungumza na nyota huyo.
Vileile kinda huyo ana uhalali wa kuchezea timu ya serbia, Belgium,Uturuki na Albania ambako mzazi wake wa kiume anapotokea.

No comments:
Post a Comment