Thursday, October 10, 2013

XAVI: LAHM ANAWEZA AKAWA KIUNGO MZURI TOFAUTI NA NAFASI ANAYOICHEZEA

Kiungo wa barcelona ya hispania Xavi Harnandez amesema kwamba nyota na kaptaini wa beryan munich Philip Lahm anaweza kuwa mchezaji mzuei zaidi pindi akicheza nafasi ya kiungo kuliko nafasi anyoichezea sasa.

Kiungo huo alisema ingawa kwa sasa nyota huyo wa timu ya taifa ya ujerumani amepata umaarufu kupitia nafasi a beki ya kulia pindi akiwa uwanjani nahata mudamwingine akichezeshwa beki wa kati , lakini kutokana na muono wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 itakuwa vizuri zaidi kama atachezeshwa nafasi ya kiungo kwa wakati huu ambapo Javi martinez ameumia.

Xavi amesema hayo baada ya kocha wake wa zamani wa barcelona Pep Guadiola kwa sasa anaifundisha Bayern Munich  alipompanga beki huyo mwenye miaka 29 katika nafasi ya kiungo kwenye mechi ya ligi kuu ya ujerumani maarufu kama bundesliga dhidi ya Liverkuse ambapo timu hizo zilitoka 1-1 baada ya viungo wa timu hiyo kuumia..

No comments:

Post a Comment