KIPA
anayeinukia vizuri nchini, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ amesikia habari
za Simba SC kusaka kipa mzuri na amesema yeye ana sifa hiyo, lakini kwa
bahati mbaya bado ana Mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya sasa,
Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro.
“Ndiyo
nimesikia na mimi hawajawahi kunifuata, ila hata wakinifuata bahati
mbaya bado hatuwezi kuzungumza kwa kuwa bado nina Mkataba wa mwaka mzima
Mtibwa, kanuni haziniruhusu kufanya mazungumzo na klabu
nyingine”alisema Cassilas alipozungumza jana usiku katika
hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es SalaCassilas
yupo katika kikosi cha pili cha timu ya taifa, Future Young Taifa Stars
kilichoweka kambi Sapphire kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya kwanza
ya taifa, leo jioni Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ni maalum kwa benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Kim Poulsen kuangalia wachezaji 10 kutoka Future Taifa Stars watakaoongezwa katika Taifa Stars tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Novemba 19 mwaka huu jijini Arusha.
Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini jana na miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuripoti ni kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia.
Mapema jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wanatafuta kipa atakayekwenda kuwa pamoja na makipa wazawa, Abuu Hashimu na Andrew Ntalla, kwa kuwa wana mpango wa kuachana na kipa Mganda, Abbel Dhaira.
“Niseme wazi, tunatafuta kipa. Huu ni mchakato makini sana na hatutaki kurudia kosa. Tunatafuta kipa mzawa, kwanza awe mwaminifu na mwenye uwezo mkubwa,”alisema.
am.
No comments:
Post a Comment