MFUNGAJI
bora wa mashindano ya Umoja na Amani, yaliyofanyika
kwenye Uwanja wa
Shule ya Msingi Ubungo Msewe, Dar es Salaam, James Msuva amesajiliwa
timu ya vijana ya Simba SC, maarufu kama Simba B na tayari amejiunga
nayo.
Mhitimu huyo wa kidato cha Nne katika sekondari ya Makongo, Dar es Salaam aling’ara katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Waziri a Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akiichezea Baruti FC.
Akizungumza jana katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es
Salaam, Msuva alisema kwamba tayari amejiunga na Simba B chini ya kocha
Suleiman Matola na amekwishaichezea mechi mbili za Ligi ya Vijana Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam na kufunga bao moja.
James aliyekwenda Sapphire jana kumtembelea kaka yake, Simon Msuva wa Yanga SC aliye kambini na timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars, alisema kwamba anamshukuru Mungu anaendelea vizuri Simba B.
“Natarajia kuichezea Simba katika mashindano ya Kombe la Uhai (michuano maalum ya timu za vijana za Ligi Kuu) na nikipata nafasi hiyo itakuwa fursa nzuri kwangu kuzidi kupambanua kipaji changu,”alisema.
Msuva mdogo aliitwa na Waziri Mukangara ofisini kwake kwa lengo la kumsaidia zaidi kumuendeleza kisoka, baada ya kuonyesha kipaji kikubwa katika michuano ya Kombe la Umoja na Amani.bao saba na kuiwezesha timu yake ya mtaani kutwaa Kombe hilo.
No comments:
Post a Comment