NAFASI
ya Sweden katika fainali zijazo za Kombe la Dunia inaweza kuwa bado ipo
shakani, lakini hiyo haijazuia Mamala ya Posta nchini humo kumpa
heshima mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic - ya kutumia picha yake katika
stempu.
Mshambuliaji
huyo wa PSG, ambaye ataongoza safu ya ushambuliaji ya nchi hiyo katika
mchezo wa kwanza wa mchujo dhidi ya Ureno Ijumaa, yupo katika zoezi la
kutengeneza aina tano za stempu ambazo zitatolewa Machi mwakani.
Ibrahimovic alisema: "Nimepata fursa ya kuwa kwenye kona ya stempu na itakuwa babu kubwa zoezi likikamilika.
"Ni heshima kubwa kuwa katika stempu ya posta, nina ninajivunia sana kuteuliwa,"
Matumaini
ya Sweden kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Brazil yapo begani mwa
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye hivi karibuni ametajwa
kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo za Mwanasoka Bora wa Dunia
2013, FIFA Ballon d'Or na tuzo ya Bora Bao la Mwaka, Puskas kutokana na
bao lakealilofunga dhidi ya England.
No comments:
Post a Comment