Friday, November 15, 2013

KIM POULSEN AMJIBU BAUSI NA KUMWAMBIA KWAMBA HAINGIZI SIASA KWENYE SOKA

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Mdenmark Kim Poulsen amemjibu kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar Salum Bausi baada ya kocha huyo kuwaita baadhi ya wachezaji wa timu ya Zanzibar wanaojiandaa na mashindano ya challenge yatakayofanyika  nchini Kenya hapo baadaye mwezi huu.

Bausi alimlaumu Poulsen baada ya kuwajumuisha baadhi ya wachezaji wa Zanzibar Mcha Viali na Mwadini na kudai kwamba anamuharibia program zake katika kujiandaa na michuani hiyo.

Poulsen aliwajumuisha wachezaji hao katika kutafuta kikosi cha kilimanjaro stars katika kujiandaa na michuano hiyo na kuwepo katika kikosi cha timu ya taifa stars kinachojulikana na ukiachia mbali kile cha young taifa stars katika program ya kocha huyo kutafuta wachezaji wa timu   hiyo kwa mashindano yajayo.

Poulsen alimwambia Bausi kwamba yeye haleti siasa katika soka na anachotakiwa yeye ni kumuita mchezaji yeyote kutoka pande zote za jamhuri ya muungano wa Tanzania pindi anapohitajika na timu hiyo na sio kuangalia anatokea wapi na kipindi gani kwani muda wowote mchezaji anatakiwa kuitwa bila ya kuzingatia anatokea wapi.

Timu ya kilimanjaro stars wapo kambini na tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya utakaofanyika Jumanne katika tarehe za fifa.

No comments:

Post a Comment