Baada ya kufanikiwa kupata saini ya goli kipa nambari moja nchini Juma Kaseja Timu ya soka na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga sports club hatimaye wamefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mahiri kutoka timu ya Ruvu Shooting inayoshiriki ligi hiyo Hassani Dilinga.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kuthibitisha swala hilo msemaji mkuu wa mabingwa hao Baraka Kizugutu amesema kwamba kweli timu hiyo imemsajili kiungo huyo na amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo.
Hata hivyo msemaji mkuu wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amesema kwamba bado hawajapata taarifa hizo na wanachoamini kwamba Hassani Dilunga bado anamkataba na timu hiyo yenye maskani mwake mkoani kibaha na mkataba alionao ni wamiaka miwili aliosaini mwanzo wa msimu huu.
Lakini kwa upande wa pili wa Yanga bado wamesisitiza kusema kwamba wamemsajili kiungo huyo kihalali na kufuata taratibu zote kwa kuwa wao wanakijuwa wanachokifanya.
No comments:
Post a Comment