USAJILI
wa dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 15 mwaka huu, Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunazikumbusha klabu zote kuheshimu
kanuni na kuzingatia muda uliowekwa.
Pia tunakumbusha kuwa kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi nafasi ya kusajili mchezaji mpya. Kama klabu ilisaji wachezaji 30 maana yake ni kuwa haina nafasi ya kuongeza wachezaji.
Kwa
upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa
kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa
sasa.
Kuhusu
usajili wa wachezaji kutoka nje mpaka sasa hakuna hata klabu moja
imeshaingia kwenye TMS kuomba uhamisho. Itakapofika Desemba 15, system
ya TMS itafunga.
Wakati
huo huo: TFF imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwamuzi wa
zamani wa FIFA, Andrew Kiloyi kilichotokea mjini Iringa.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Mkoa wa
Iringa, Ramadhan Mahano, Kiloyi alifariki dunia juzi (Novemba 24 mwaka
huu) kutoka na ugonjwa wa fangasi ya ubongo, na marehemu amesafirishwa
kwenda kwao Kigoma ambapo atazikwa.
Kiloyi alizaliwa Mei 5, 1968. Alijiunga na uamuzi wa mpira wa miguu mwaka 1988 ambapo alipata beji ya FIFA mwaka 2001 akiwa mwamuzi msaidizi. Alistaafu uamuzi mwaka 2009, na hadi anafariki akiwa mjumbe wa Kamati ya Waamuzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IREFA).
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pole kwa familia ya marehemu, IREFA, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwataka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hicho cha majonzi. Mungu aiweka mahali pema roho ya marehemu Kiloyi.
No comments:
Post a Comment