Thursday, December 5, 2013

KIIZA AFIWA NA BABA YAKE UGANDA

MSHAMBULIAJI wa Uganda, The Cranes, Hamisi Friday Kiiza maarufu Diego, amepokea habari mbaya akiwa Kenya kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.

Habari hizo ni kufiwa na baba yake mdogo, ambaye ndiye aliyemlea vyema hadi kuwa Kiiza Diego huyu ambaye leo anawapa raha Waganda.

Mshambuliaji huyo wa Yanga SC ya Tanzania amesema kwamba baba yake huyo amefariki leo asubuhi mjini Kampala Uganda.
“Nimeumia sana, lakini uongozi wa timu umesema nisubiri hadi tumalize mashindano, sina jinsi, lakini ni msiba mkubwa kwangu, kwa sababu yule ndiye baba aliyenilea,”alisema.

 
Kiiza aliingia kipindi cha pili wakati Uganda inaifunga Sudan 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi C na kutinga Robo Fainali kwa ushindi wa asilimia 100, baada ya awali kuzifunga Rwanda 1-0 na Eritrea 3-0.

 
Uganda sasa itamenyana na Tanzania Bara Jumamosi katika Robo Fainali ya Kwanza Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya.

No comments:

Post a Comment