Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya soka ya Eritrea,
wameripotiwa kutoweka nchini Kenya huku michuano ya CECAFA ikiendelea
nchini humo.
Wawili hao wanasemekana huenda wakaomba hifadhi nchini humo.
Sio
mara ya kwanza kwa wachezaji wa timu hiyo kupotea wakiwa katika nchi ya
kigeni kushiriki michunao ya kikanda. Eritrea ni moja ya nchi zenye
ukandamizaji mkubwa wa kisiasa barani Afrika.
Mwezi Disemba mwaka jana, wachezaji 17 wa timu
hiyo pamoja na daktari wao waliomba hifadhi nchini Uganda , miezi minane
tu baada ya wachezaji wengine 13 kutoka katika klabu moja ya nchi humo
kuomba hifadhi nchini Tanzania.
Mwaka 2009,wachezaji wengine wa timu ya taifa ya Eritrea walipotelea nchini Kenya.
''Hili ni jambo la kusikitisha sana kwa tukio
kama hili kutokea tena, na inasababisha wasiwasi kwa maafisa wa soka
kanda ya Afrika Mashariki na Kati,'' alisema Nicholas Musonye, katibu
mkuu wa (Cecafa).
Wachezahi hao wawili, ambao wangali kutajwa,
walikosa kurejea katika hoteli yao siku ya Jumamosi baada ya kutizama
mechi nyingine.
Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa
Mataifa, Navi Pillay, mwaka jana aliituhumu serikali ya Eritrea kwa
kuwaua watu wasio na hatia, mateso na kuwazuilia maelfu ya wafungwa wa
kisiasa.
Maelfu ya watu nchini Eritrea, hujaribu
kuitoroka nchi hiyo, kila mwaka huku wengi wakifariki katika safari yao
bahari kukimbilia ulaya
No comments:
Post a Comment