HELIKOPTA ilitu uwanjani kubeba majeruhi baada ya kutokea vurugu katika mechi ya soka Brazil jukwaani baina ya mashabiki.
Mchezo kati Atletico PR na Vasco da Gama, ulisimamishwa Jumapili baada ya mashabiki kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Mashabiki waliokuwa wanapigana ilibidi watenganishwe na Polisi wa kutuliza ghasia kwa kuwafyatulia mabomu.
Mchezo huo ukaanza tena baada ya saa moja na dakika 10 za kusimama kupisha vurumai.
Tukio hili ni baya kwa Brazil, na litaifanya nchi hiyo ijipange kwa matukio ya aina hiyo wakati wa Fainali za Kombe la Dunia.
Hatari: Vurugu zilizotokea jukwaani baina ya mashabiki zilisababisha helikopta itue kuchukua majeruhi
Mashabiki waliojeruhiwa wakibebwa kupelekwa kwenye helikopta
Wanatenganishwa: Polisi waliwafyatulia mabomu mashabiki ili kuwatenganisha
Mashabiki wa Atletico wakimtimba mateke shabiki wa Vasco da Gama
Hofu: Binti aliyeshika mpira akilia wakati wa vurugu hizo
Helikopta ilitua uwanjani kuokoa majeruhi
Mashabiki wakichukuliwa ajili ya huduma ya kwanza baada ya kuumia
Hii ni kuashiria tahadhari kubwa inapaswa k
No comments:
Post a Comment