HATUA
ya makundi ya Kombe la Mapinduzi imehitimishwa usiku huu kwa mchezo wa
mwisho wa Kundi C, Azam FC ikiilaza Ashanti United bao 1-0 Uwanja wa
Amaan, Zanzibar.
Bao
pekee la Azam leo limefungwa na Mganda, Brian Umony dakika ya 60,
akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche kutoka wingi ya kulia.
Kwa
matokeo hayo, Ashanti inayofundishwa na kocha mkongwe, Alhaj Abdallah
Athumani Seif ‘King Kibaden’ inaaga mashindano haya. Ashanti ilihitaji
sare tu katika mchezo wa leo ili ifuzu Robo Fainali, lakini imalambwa
kidude.
Kipre Tchetche akimpongeza Brian Umony baada ya kufunga leo Uwanja wa Amaan |
Timu
zilizofanikiwa kuingia Robo Fainali ni Azam FC na Tusker ya Kenya
kutoka Kundi C, Simba SC na KCC ya Uganda kutoka Kundi B, URA ya Uganda,
Chuoni, Cloves Stars na KMKM.
Robo
Fainali zitachezwa Jumatano, Tusker na URA Saa 8:00 mchana na Azam FC
na Cloves Saa 10:00 jioni Uwanja wa Gombani Pemba na Uwanja wa Amaan,
mechi ya kwanza itakuwa kati ya KCC na KMKM Saa 10:00 na Simba SC na
Chuoni Saa 2:00 Usiku.
PICHA KWA MSAADA WA BINZUBEIRY BLOG
No comments:
Post a Comment