KLABU
ya Manchester United imepiga hatua katika harakati zake za kusaka za
kuimarisha kikosi chake baada ya kwenda kuwatazama Diego Costa na Ander
Herrera mwishoni mwa wiki.
Baada
ya kutolewa kwenye Kombe la FA na Swansea, kipigo ambacho ni mwendelezo
wa msimu mbaya United, kocha David Moyes amesema kwamba kuna jitihada
za dhati klabu hiyo ya Old Trafford kusajili wachezaji.
Amekuwa akisaka beki wa kushoto, kiungo na mshambuliaji Ulaya mzima.
Diego Costa aliiwezesha Atletico kupanda kileleni mwa La Liga baada ya kuifunga Malaga 1-0
Msaka
vipaji mkuu wa United, Robbie Cooke alimshuhudia mchezaji wa bei ghali
Costa akicheza dakika zote 90 huku Atletico Madrid ikishinda 1-0 dhidi
ya Malaga Jumamosi.
Koke
– mchezaji ambaye United wamekuwa wakihusishwa naye lakini hawana nia
ya kumsajili mwezi huu – alifunga bao pekee kwenymchezo huo.
Cooke
alikuwa mmoja wa watu wa benchi la Ufundi walioambatana na Moyes kutua
Old Trafford wakitokea Everton na mpango huo ulimfanya asafiri kutoka
pwani ya kusini ya Hispania hadi kaskazini mwa San Sebastian,
kumuangalia mchezaji wa Atletico Bilbao, Herrara akicheza mechi ya
kipigo cha 2-0 kwa Real Sociedad.
Costa,
ambaye pia alitakiwa na Liverpool Agosti mwaka jana na hivi karibuni
amekuwa akihusishwa na kuhamia Chelsea na Arsenal, amekuwa mmoja wa
washambuliaji gumzo Ulaya msimu huu, baada ya kufunga mabao 19 katika
mechi 18 na kuisaidia timu yake kuwa mpinzani mkuu wa Barcelona katika
mbio za ubingwa wa La Liga.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyekataa ofa ya uraia wa Hispania mwaka
jana ili aichezee Brazil katika Kombe la Dunia, nchi yake halisi
aliyozaliwa, alisaini Mkataba mpya na Atletico ili kumzuia kwenda
Liverpool, lakini anaweza kuuzwa kwa Pauni Milioni 31.
No comments:
Post a Comment