Tuesday, January 7, 2014

MASHETANI BADO YAZIDI KUMSUMBUA MOYES

Suala hapo lipo wazi sana ... Wenye upeo na wasiotekwa na mapenzi na timu iyo waliona tangu msimu uliopita ila wale walio wenzangu wenye mahaba niue wakaona timu yao inanguvu...

Msimu uliopita Manchester ilichukua taji, kwakua Rooney na van persie walikua wapo vizuri hasa van persie hakupata maumivu ya mara kwa mara ila kiujumla team iyo ilikua ya kawaida sana kwa wachezaji ambao ferguson Alikua ana watumia ...

Nakumbuka shafih dauda alisema iyo team ina mwili wa baunsa mbele ina forward kali ila kuanzia kwenye midfield ya chini na mabeki wake ni dhaifu .. Watu mkamtukana sana ...

Ferguson alilijua hilo suala kua kikosi chake anachotumia ni cha kawaida na sehemu ya defensive ya team iyo kuanzia kiungoni ni dhaifu alichokua anafanya ili kuficha madhaifu Alikua wakicheza mechi team yote anaiweka nyuma ili wasiruhusu goli huku wakitumia strikers zao wawili world class Rooney na van persie kuwapa matokeo , na Alikua akishapata ushindi Alikua hafunguki tena kushambulia .. Sio siri msimu ulipita united ilichukua ubingwa huku ikiwa inacheza mpira wa ovyo sana ila hamkuliona hilo kwakua mlikua mnapata ushindi ...

Huyu David Moyes amekuja na gundu kwanza kabisa Kuyumba kwa van persie kimajeruhi, na pili anatumia team ile ile ya Ferguson wachezaji wale wale ila tatizo lake yeye anataka kufunguka ashambulie muda wote Wakati wachezaji hana wa kufanya hivyo mwisho wa siku anaanza kufungwa yeye na kuanza kupata Shida ya kusawazisha, Ferguson mwenzake Alikua anaiweka team nyuma anaacha van persie na Rooney wafanye yao ila hakua anapandisha team yote kama moyes, Ferguson Alikua afungui uwanja hivi ....

Hiyo team hata haihitaji hata mabadiliko sana kuna wachezaji, humo humo ndani ya team wana hitaji kuaminiwa wapate nafasi za kucheza wanaweza kuleta utofauti, na pia David Moyes anasema hamna watu wa kuwasajili Wakati kuna kuna mafundi kibao tu wapo team za kawaida wanaoweza kuongeza kitu kipya kwenye team ... Kwa mfano Oscar wa Chelsea watu wamemsajili kutoka kwao brazil kaja kufanya mambo hata hakutoka kwenye team kubwa za ulaya ... Fernandinho wamemtoa shaktar donest team isiyoweza kuvumilia offer kutoka team kubwa.

Mimi nina sema Combination ya Rooney na van persie ni combination hatari zaid kuliko hata zlatan na cavan, negredo na aguero au suarez na sturridge ... ila Rooney na van persie msimu huu wanatumia muda mwingi kufanya kazi ya viungo wao kuliko kufunga magoli ....

Wilfred Zaha Mchezaji Bora Championship mara mbili mfululizo sidhani kama angeshindwa kucheza vizuri kama angeaminiwa, kwa sasa hivi anavyocheza mechi moja kwa miezi miwili ni kumfanya asijiamini uwanjani na kuogopa zaid kuharibu ....

Na pale wapo wengi tu kwenye janga hili, hawa akina Anderson na Kagawa hawaaminiwi kwenye mechi za kawaida wanakuja kupangwa kwenye mechi zilizo very trick alafu wakicheza ovyo wanasugua benchi muda mrefu ....

United itasimama tena kama wakiamua kusimama tena ila kama akiendelea kuwatumia wachezaji wale wale vipenzi vya Ferguson ataua iyo team kwakua yeye Moyes Sio Ferguson hawezi kuchimba matokeo ya ushindi kama hata team ikiwa mbovu...

No comments:

Post a Comment