Saturday, January 4, 2014

SIMBA YALAZIMISHWA SARE JANA DHIDI YA KCC YA UGANDA

SIMBA SC imegawana pointi na KCC ya Uganda baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Kwa ujumla timu zote zilitoshana nguvu na maarifa kwa dakika zote 90 za mchezo huo, huku makipa wote, Ivo Mapunda wa Simba na Magoola Omar wa KCC 
wakistahili sifa kwa kuokoa michomo mingi ya hatari. Mabeki wa KCC walimdhibiti vizuri winga machachari wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ leo, wakati pia beki Mkenya, Donald Mosoti Omwanwa aliiongoza vyema safu ya ulinzi ya Simba SC. 
Kipa wa KCC, Magoola Omar akiruka juu kupangua mpira kichwani kwa mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki jioni hii Uwanja wa Amaan
Matokeo hayo yanazifanya Simba SC na KCC ziendelee kukabana kileleni, kila timu ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi mbili. Mapema jioni katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, wenyeji KMKM nao walitoshana nguvu na AFC Leopard ya Kenya kwa sare ya 0-0 pia. Mechi za Kundi B zitahitimishwa Januari 5, kwa Simba kumenyana na KMKM na KCC na Leopard. Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi C, Ashanti ikimenyana na Spice Stars na Azam FC na Tusker ya Kenya Uwanja wa Amaan, wakati Uwanja wa Gombani, Pemba Clove Stars itamenyana na URA ya Uganda na Mbeya City na Chuoni.
  Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, 

Ramadhani Singano/Zahor Pazi dk89, Amri Kiemba/Said Ndemla dk50, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk67, Uhuru Suleiman/Ramadhani Chombo dk48 na Haroun Chanongo/Edward Christopher dk78. 
  KCC; Magoola Omar, Saki Mpima, Kavuma Habibu, Kawooya Fahad, Kiiza Ibrahim, Senkumba Hakim, Waswa Herman, Masiko Tom, Tony Odur, Stephen Bengo/Gadafi Kiwanuka dk 58 na Wadri William. 

picha kwa msaada wa Binzubeiry blog

No comments:

Post a Comment