Saturday, June 6, 2015


DE GEA AWAAGHA WENZAKE MAN UNITED

KWAHERI: David De Gea awaaga wenzake Old Trafford


MIKONO ya kipa, David de Gea, iliyotumika kuibeba Man United katika msimu uliomalizika hivi karibuni, inadaiwa kuwa imetumika pia kuwaaga wachezaji wenzake kikosini humo hivi karibuni katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Carrington.
Inadaiwa kipa huyo hataivaa tena jezi ya Man United na ripoti za England zinadai ameshawaaga wachezaji wenzake, benchi la ufundi na wafanyakazi wa klabu.
Staa huyo aliyenunuliwa kwa Pauni 18 milioni Juni 2011 na kuwa kipa ghali England, amegoma kusaini mkataba mpya Old Trafford ambao ungemfanya awe analipwa Pauni 200,000 kwa wiki.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anaamini atampata De Gea kwa Pauni 25 milioni tu kwa kuwa mkataba wake Old Trafford umebakiza miezi 14 na kipa huyo mzaliwa wa Madrid, amedhamiria kurudi katika jiji hilo ambalo ni makazi ya mpenzi wake, Edurne Garcia Almagro, staa wa muziki wa Pop.
Madrid ilikuwa inasubiri imalize suala lake la kuachana na kocha, Carlo Ancelotti, kabla ya kumgeukia De Gea ambaye atakuwa mbadala wa muda mrefu wa kipa wao, Iker Casillas, ambaye nyakati zinaonekana kumpita.
Kocha wa Man United, Louis van Gaal, ambaye yupo likizoni Ureno, amekiri hana ubavu wa kumzuia kipa huyo asiondoke kurudi kwao Hispania.
“Sidhani kama ninaweza kumshawishi abaki kwani anajua kila kitu ilichonacho Man United. Sihitaji kusema lolote, yeye mwenyewe anahisi kila kitu. Umewaona mashabiki (wanavyompenda) inashangaza sana. Atakapoondoka, atapoteza hilo. Ana sifa nyingi. Inabidi aamue mwenyewe,” alisema Van Gaal.
Licha ya kubembelezwa kiaina na Van Gaal, De Gea ametoa kauli inayoashiria kwamba ataondoka baada ya kutotaka kuzungumzia hali yake ya baadaye huku akisisitiza yuko likizo kwa sasa.

ZIJUE A,K,A ZA WACHEZAJI TOFAUTI WA BONGO WAKIJIFANANISHA NA WA NCHI ZA NJE .. SWALI LA KUJIULIZA JE KWELI WANAENDANA?

Unawajua Cannavaro, Boban, Nemanja Vidic, Garincha, Fabregas, Barthez wa Bongo? Wasome hapa
SOKA la Tanzania limekuwa likipiga hatua siku hadi siku na hiyo inatokana na kuibuka kwa vipija vingi vya vijana ambao wanavutiwa na mchezo huo unaoongoza kuwa na mashabiki wengi duniani.
Utaditi uliofanywa na Goal unaonyesha asilimia 65 ya vijana wa kiume wa Tanzania wanapenda mchezo wa soka na wengi wao wamejiingiza kwenye mchezo huo kama siyo kwa kuucheza basi kwa kushangilia timu mbalimba iwe za ndani au za Barani Ulaya.

Kutokana na soka kuwa mchezo maarufu kupita yote duniani na ukiongeza na utandawazi uliopo kupitia Televisheni hata wachezaji wakubwa wanaocheza timu zinazo shiriki ligi kuu ya Vodacom wamekuwa ni wafuatiliaji wa zuri wa ligi za Ulaya na wengine kutokana na uhodari wame wamepachikwa majina ya utani ya wachezaji wa Ulaya na mashabiki wao na wengine wamejipa wao wenyewe.
Hapa chini Mtandao wa Goal unakuletea wachezaji nane wenye umaarufu mkubwa katika Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutumia AKA za majina ya wachezaji wa Ulaya kiasi cha majina yao halisi kutofahamika kwa mashabiki.

1.Nadir Haroub ‘Cannavaro huyu ni nahodha wa klabu kubwa Tanzania inayoongoza ligi kuu ya Vodacom na pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutokana na nafasi anayocheza uwanjani na mchango wake kwa timu hizo mbili amebatizwa jina la nahodha wa timu ya taifa ya Italia Fabio Cannavaro.
Mchango wa Hadir Haroub kwa timu hizi mbili haupishani sana na Cannavaro halisi wa Italia kwani amekuwa akicheza kwa bidii ya hali ya juu na wakati mwingine ameweza kuifungia timu yake mabao mahimu katika mechi muhimu na pindi anapokosekana labda kwa matatizo ya majeruhi ama kutumikia adhabu basi hali huwa tete na hofu huongezeka kwa mashabiki wake.

2.Haruna Moshi ‘Boban’ huyu ni kiungo mshambuliaji wa timu ya Friends Rangars zamani aliwahi kutamba na klabu kubwa ya Simba na hata Coastal Union alipewa jina la Boban na mashabiki wa SImba kutokana na uwezo wake anapokuwa dimbani ambao ulikuwa ukifanana na ule wa Mcroatia Zvonimir Boban aliyetamba na klabu ya AC Milani ya Italia.

Mbali ya uwezo wake awapo dimbani lakini Boban wa Tanzania amekuwa na vituko vingi ambavyo vinamfanya awe mchezaji wakipee nchini na haikushangaza Agosti 2010 alipovunja mkataba na timu ya Gavle IF, ya Sweden aliyokuwa anaichezea kama Profeshino.

3.Kelvin Yondani , ‘Nemanja Vidic’ Huyu ni beki mwingine mwenye jina kubwa kwenye ligi ya Tanzania bara akiichezea Yanga na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ uwezo wake wa kuwadhibiti washambuliaji hatari mashabiki wake wakati huo akiichezea Simba walimpa jina hilo wakimfananisha na Vidic ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Inter Millan ya Italia akitokea Mancherster United.
Sifa kubwa aliyokuwa nayo Yondan na kusababisha mashabiki hao kumfananisha na Vidic ni jitihada zake anazozifanya uwanjani za kulinda lango lake huku akiruka vichwa kwa kufunga au kuokoa kama ilivyo kwa mwenye jina hilo Mserbia Nemanja Vidic .

4.Steven Mapunda ‘Garincha’ Huyu ni winga wa zamani aliyewahi kutamba na klabu ya Simba na kidogo timu ya taifa ‘Taifa Stars kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kupiga chenga akiwa kwenye kasi mashabiki wa soka walimbatiza jina la Garincha akifanianishwa na Mbrazili Manuel Francisco dos Santos
Uwezo wa mchezaji huyo aliyetamba na timu ya Brazili ulikuwa ni hatari kwa mabeki wa timu pinzani sawa na Mapunda ambaye kwa sasa ameshastaafu soka na yupo kwao Songea anaendeleza kipaji chake kwa kuibua vipaji vya soka.

5.Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ Kiungo fundi raia wa Rwanda anayecheza soka la profeshino kwenye klabu ya Yanga ya Tanzania ni mmoja ya wachezaji maarufu Afrika Mashariki na Kati na kiwango chake cha kuichezesha timu na kutoa pasi za mabao kumewafanya mashabiki wa soka wa Rwanda kumpachika jina la kiungo huyo anayeichezea klabu ya Chalsea ya Uingereza kwa sasa.
Uwezo wa Niyonzima mbaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ umeweza kuwavutia makocha wengi ambao wamekuwa wakimuhitaji kwa ajili ya kuzitumikia timu zao na huenda mwishoni mwa msimu huu kiungo huyo akaachana na Yanga na kurudi kwao Rwanda kuichezea APR kwani amegoma kuongeza kusaini mkataba mpya.

6.Wazir Mahadhi ‘Mendieta’ Huyu ni kiungo wazamani wa Tanzania aliyepata umaarufu mkubwa wakati akiichezea klabu ya Yanga kutokana na uwezo wake mashabiki wa soka waliamua kumpa jina la kiungo wa Hispania Gaizka Mendieta ambaye kwa sasa amestaafu soka .
Mara ya mwisho Wazir Mahadhi kuchezea timu za ligi kuu ya Vodacom ilikuwa ni msimu wa 2009/2010, wakati aliposajiliwa na Moro United na kuonyesha uwezo mkubwa pamoja na ukongwe aliokuwa nao lakini pamoja na mchango mkubwa timu hiyo ilishuka daraja mwishoni mwa msimu na yeye kuamua kustaafu rasmi kucheza soka.

7.Ally Mustaph ‘Barthez’ Huyu ni kipa changuo la kwanza kwa sasa kwenye klabu ya Yanga ambaye uwezo wake wakati huo akiichezea Ashanti ya Ilala 2006 ulisababisha mashabiki wa timu hiyo kumpachika jina la Fabian Barthez kipa wa Ufaransa na klabu ya Manchester United aliyefanya vizuri kwenye fainali za kombe la Dunia za mwaka 1998.
Jina la Barthez limemsaidia sana kipa huyo wa Tanzania kudumu kwenye soka kutokana na kupitia kwenye vipindi vigumu ikiwemo kukaa benchi kwa msimu mzima wakati alipohamia Simba huku kipa namba moja wakati huo akiwa Juma Kaseja, lakini uvumilivu wake ulikwisha baada ya kuhamia Yanga misimu mitatu mitatu iliyopita na kuipa ubingwa Yanga katika msimu wa kwanza lakini napo alipata matatizo baada ya kufungwa mabao matatu dhidi ya timu yake ya zamani Simba na kuwekwa benchi kwa muda mrefu kabla ya kupambana na kurudi kwenye nafasi yake.

8.Deogratius Munish ‘Dida’ Kama ilivyo kwa Batherz Munish naye ni mmoja wa makipa hodari anayeichezea klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ uwezo wake akiwa na klabu za Simba, Mtibwa Sugar, Azam FC na sasa Yanga pamoja na urefu wake mashabiki walimpachika jina la DIDA wakimfananisha na kipa wa Brazili Nélson de Jesus da Silva aliyepata umaarufu mkubwa akiwa na klabu ya AC Millan ya Italia.
Ingawa Dida wa Brazili kwa sasa hana jina baada ya kurudi kucheza ligi ya kwao katika timu ya Sport Club Internacional lakini Dida wa Yanga bado yupo kwenye kiwango licha ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza na hiyo ilitokana na uzembe alioufanya kwenye baadhi ya mechi na kocha Hans van der Pluijm kumpa nafasi Barthez.
Utumiaji wa majina hayo kumekuwa kukiongeza hamasa kubwa kwenye mechi za Ligi Kuu kwa sababu wachezaji hao wanalazimika kujituma zaidi kuonyesha tofauti na wengine kutokana na kufahamika zaidi na wakati mwingine kulinda heshima ya majina wanayoyatumia kwa kuonekana wapo juu kila siku.

NNI HATIMA YA DI MARIA NDANI YA MANCHESTER UNITED? FUATILIA MWENYEWE ALIVYOSEMA JANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Angel Di Maria amekanusha tetesi zinazoeleza kuwa yupo katika mpango wa kutimka Manchester United na amesisitiza kuwa atarudi Old Trafford msimu ujao.

Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alijiunga na Man United kwa ada ya usajili ya paundi milioni 59.7 akitokea Real Madrid na kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza, lakini ameshindwa kuonesha cheche katika msimu wake wa kwanza.

Di Maria ambaye yupo na timu ya taifa ya Argentina inayocheza michuano ya Copa America amesema hana mpango wa kuondoka Man United na anatarajia kurudisha kiwango chake msimu ujao chini ya Louis van Gaal.

“Nimemaliza msimu wangu wa kwanza kuichezea Manchester United,” Amewaambia The Sun. “Ulikuwa msimu mgumu kwangu. Nadhani ulikuwa mgumu kwasababu ilikuwa ni taifa lingine na klabu nyingine, ligi hii ni ngumu kuliko ya Hispania. Sikuweza kuendana nayo kwa haraka”.

Sasa nitacheza Copa America na kurudi kucheza Manchester United msimu wangu wa pili, nadhani nitarudi kwenye ubora wangu”.

Kiufupi tu ni kwamba Angel Di Maria amefanikiwa kuchukuwa tuzo baada ya goli lake alilofunga dhidi ya Liecester City kuchaguliwa kuwa gili bora la msimu baada ya kumpiku Chalie Adam na goli lake alilofunga dhidi ya chelsea kwa msimu uliopita wa ligi 2014-2015. .

KUMEKUCHAAA!!!! BARCELONA NA JUVENTUS WAKIWASILI UJERUMANI... WEKA KURA YAKO SASA NANI KUIBUKA NA USHINDI?


SAKATA LA MESSI NA SIMBA LAFIKIA PATAMU, TFF YATAKA KUKUTANA NAO





TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba.
TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo. 
Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake. 
Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.
 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)