KIUNGO
nyota wa Simba SC, Ramadhani Yahay Singano ‘Messi’ leo asubuhi aliwekwa
kikao cha dharula na viongozi wa klabu yake, kwa kuonyesha kitendo cha
utovu wa nidhamu wakati wa safari ya timu hiyo visiwani Zanziabr kwenye
Kombe la Mapinduzi.
Wachezaji
wa Simba SC wakiwa bandari ndogo ya Azam Marine, Dar es Salaam asubuhi
tayari kwa safari ya Zanzibar, Messi alifika akiwa hana jezi ambayo
wachezaji waliagizwa wavae wakati wa safari.
Kitendo hicho kiliwaudhi Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC waliokuwa wanaongoza msafara, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na Said Pamba ambao walilazimika kumuita pembeni mchezaji huyo kumuhoji.
Baada ya utetezi wake, ilibidi na Meneja wa timu, Mganda Moses Basena aitwe kutoa ushahidi. Hata hivyo, Basena alionekana kutokubaliana na maelezo ya Messi, lakini viongozi wakaachana naye aendelee na safari.
Messi amekuwa kipenzi cha wana Simba SC tangu Desemba 21, mwaka huu acheze kwa kiwango cha juu katika mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga wa Nani Mtani Jembe na kusaidia ushindi wa mabao 3-1.
Inaonekana kama sifa alizozipata baada ya mchezo huo, zinaanza kumfanya ajione yuko tofauti na wachezaji na wenzake, jambo ambalo viongozi wa klabu hiyo wanaonekana mapema kuanza kupambana nalo.