Monday, September 30, 2013

TAARIFA KUHUSU UJENZI WA UWANJA WA YANGA SPORT CLUB

LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana

Mara ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.

Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:

· Kupata na kuwa na eneo la kutoshereza malengo ya mradi

· Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na mkandarasi mzuri wa mradi

· Kupata na kutenga fedha za kukamilisha usanifu na ujenzi wa mradi

Kwa upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.

Kutokana na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-

1. Uwanja wa mpira wenye viti 40,000

2. Hostel ya wachezaji na football academy ya vijana

3. Viwanja vya mazoezi

4. Uwanja wa kutosha kuegesha magari

5. ­­­­­Hoteli na sehemu ya makazi

6. Ukumbi wa mikutano

7. Sehemu ya maofisi, benki, zahanati (sports clinic)

8. Maduka, supermarket na sinema

9. Sehemu za kubarizi, kupumzikia (Recretional and Open spaces)

Mara baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City” na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na kitalii.

Ili kukamilisha azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.

Mwezi wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Klabu ya Yanga ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na haba hujaza kibaba.

Ndugu Wandishi wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu kuhusu michoro ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi na BCEG limesimama, likisubiri majibu ya nyongeza la eneo. Ni matumaini yetu zoezi hili litakamilika hivi karibuni na kuendelea na mradi.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO

Dar es Salaam, 30 September 2013

Francis Mponjoli Kifukwe

RATIBA: HII NDIYO MICHEZO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA WIKI HII

Tuesday 01 October 2013
Zenit St PetersburgvFK Austria WienPetrovski Stadium18:00
ArsenalvNapoliEmirates Stadium20:45
Borussia DortmundvMarseilleSignal Iduna Park20:45
CelticvBarcelonaCeltic Park20:45
FC PortovAtltico de MadridEstadio do Dragao20:45
Steaua BucharestvChelseaStadionul Ghencea20:45
BaselvFC Schalke 04St Jakob-Park20:45
AjaxvMilanAmsterdam Arena20:45
Wednesday 02 October 2013
CSKA MoscowvViktoria PlzenArena Khimki18:00
Paris Saint GermainvBenficaParc des Princes20:45
Bayer 04 LeverkusenvReal SociedadBayArena20:45
JuventusvGalatasarayJuventus Stadium20:45
RSC AnderlechtvOlympiakosConstant Vanden Stock20:45
Real MadridvFC KbenhavnSantiagoBernabu20:45
Shakhtar DonetskvManchester UnitedDonbass Arena20:45
Manchester CityvFC Bayern MnchenEtihad Stadium20:45

MANCINI AMFUATA DROGBA GALATASARAY

Timu ya galatasaray ya uturuki hatimye imefikia muafaka na kumalizana na kocha aliyetimuliwa katika timu ya manchester city may mwaka huu Robato Mancini.

Uongozi wa timu hiyo umefikia makubaliano na kocha huyo kuifundisha kwa muda wa miaka mitatu ili kujiweka vizuri katika ramani ya soka barani ulaya.

Kocha huyo aliyewahi kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya italia kwa miaka mitatu na kombe la ligi kuu ya uingereza akiwa na manchester city pamoja na kombe la FA.

Uongozi wa tmu hiyo umechukuwa maamuzi ya kumchukuwa kocha huyo baada ya kumtimua kocha wake kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyoambapo hadi sasa imeshinda mechi moja tu kati ya sita walizpcheza.


Sunday, September 29, 2013

VIDEO: LIVERPOOL IKIICHAPA SUNDERLAND 3-1 LEO, SUAREZ APIGA MBILI

SMBA MWENDO MDUNDO LIGI KUU BARA YAICHAPA JKT RUVU 2-0 UWANJA WA TAIFA

Simba sports club imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mashindano ya ligi kuu ya Tanzania bara inayojulikana kama Vodacom Primier league.

Timu hiyo ya simba imefanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Ilichukuwa dakika ya 25 pale beki wa jkt ruvu alipounawa mpira ndani ya eneo la hatari ndipo mwamuzi wa mchezo huwo kuamuru penalti ipigwe katika dakika ya 26.
Alikuwa mfmania nyavu maarufu tangu ligi kuu ianxe wa timu ya simba Amisi Tambwe alipokwenda kupiga penalt  na kuiandikia bao la kwanza  na kumuacha kipa wa jkt ruvu shabani dihile akiruka bila ya mafanikio.

Hadi mwamuzi anapiliza kipyenga kuamuru mchezo ni mapumziko na simba ilikuwa kifuambele kwa bao 1-0. Baada ya kipindi cha pili kuanza ilchukuwa dakika 30 tu ndipo mchezaji kinda wa timu hiyo ramadhan singano alipoingia kuchukuwa nafasi ya Amri Kiemba na kuiandikia goli la pili baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa mombeki.

Mpaka dakika ya mwisho wa mchezo huwo simba wakatoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

WAKATI HUO HUO:

Ligi hiyo iliendelea katika viwanja vingine ambapo katika uwanja wa sokoine mjini mbeya timu ya Azam alitoka sare ya nao 1-1 dhidi ya Prisons ya mbeya, pia katika uwanja wa chamanzi timu za mtibwa sugar na ashant united ya da es salaam walotoka sare ya mabao 2-2.

VIDEO:REAL MADRID AKICHAPWA NA ATHLETICO MADRID 1-0

LIONEL MESSI NJE WIKI TATU

Mshambuliaji hatari Lionel Messi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina amepata majeruhi na atakaa nje kwa kipindi cha wiki mbili au tatu.

Kwa mujibu wa madaaktari  na uongozi wa timu hio umebainisha kwamba nyota huyo atakaa nje kwa kipindi hicho.

Lionel messi aliyapata majeruhi baada ya kufunga goli dhidi ya almenia katika dakika ya 21 ya mchezo huwo .


Nyota huyo itabidi apone haraka kwani timu yake inakaribiwa na michezo migumu iiwemo ya ligi kuu na ligi ya mabingwa arani ulaya, kwani kwa haraka anaweza kuzikosa mechi dhidi ya glascow celtic na villadoid,

Hata iyo messi anatarajiwa kurudi uwanjani wakati timu yake itakapomenyana na osasuna oktpber 19 katika mchezo wa ligi kuu na baadaye dhidi ya real madrid. oktober 26.


MOYES AWASHUSHA PRESHA MASHABIKI KUHUSU KAGAWA

Bosi wa manchester united David moyes amewashusha presha mashabiki kuhusiana na nyot raia wa japani shinji kagawa .

moyes amesema kwamba kagawa yupo kwenye malengo yangu ya baadaye japokuwa alimtoa baada ya kumalizika kipindi cha kwanza na kuingia Januzaj katika mechi ya ligi kuu ya englanda dhidi ya WBA ambayo iliisha kwa manchester united kupoteza mchezo huo.

Nyota huyo ambaye ameshaonekana mara 20 na kufumga mabao 6 ya ligi kuu alitolewa jana katika mechi hiyo japokuwa alicheza vizuri na kusaidiwa na nyota kijana Adnan Januzaj.

aliongeza kwa kusema shinji na mchezaji anaecheza nafasi ya namba 10 uwanjani lakini kwa sasa tunamchezesha namba ambaye sio kwake kutokana kuwepo watu wa namba hiyo na na nitamfanya awemchezaji w kikosi cha kwanza kwani bado najaibu kumtazama nini anachofanya na nishakiona.

VIDEO: MACHESTER ILIVYO CHAPWA BAO 2-1 NA WBA

Friday, September 27, 2013

HII NDIYO RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA WIKI HII


All times CAT (SA, GMT+2)
Saturday 28 September 2013
Tottenham HotspurvChelseaWhite Hart Lane13:45
Aston VillavManchester CityVilla Park16:00
FulhamvCardiff CityCraven Cottage16:00
Hull CityvWest Ham UnitedThe KC Stadium16:00
Manchester UnitedvWest Bromwich AlbionOld Trafford16:00
SouthamptonvCrystal PalaceSt. Mary's Stadium16:00
Swansea CityvArsenalLiberty Stadium18:30
Sunday 29 September 2013
Stoke CityvNorwich CityBritannia Stadium14:30
SunderlandvLiverpoolStadium of Light17:00
Monday 30 September 2013
EvertonvNewcastle UnitedGoodison Park21:00

MOYES: ROBIN VAN PERSIE YUKO TAYARI KUIKABILI WBA KESHO

Kocha wa timu ya manchester united David  Moyes amesema kwamba mshambuliaji wake hatari na ni namba moja kwa kupachika mabao Robon Van Persie yuko tayari kuikabiri timu ya West Bromwich Albion kesho kwenye ligi kuu nchini humo.

Mchezo huo utakaofanyika katika dimba la nyumbani la old trafford katika mishale ya saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki

Kwa mujibu wa kocha huyo ni kwa mba mchezaji huyo yuko tayari kwa mchezo huwo baada ya kupona jeraha alilopata wiki moja iliyopita na kumfanya aikose mechi ya upinzani dhidi ya manchester city ambapo united walifungwa 4-1.

Moyes aliendelea kusema kamba bado mchezaji mmoja tu ambaye ni majeruhi ambae ni kiungo Tom Cleverly na kwa sababu hiyo ataikosa mechi hiyo ambayo ni muhimu kwa yunited kushinda

NGASSA AWALIPA FEDHA SIMBA NA KUWASHUSHIA MANENO MAZITO

Baada ya kuwalipa simba fedha taslimu kiasi cha shilingi millioni 45 alizodaiwa kuwalipa timu hiyo baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa mechi sita kutocheza za ligi kuu ya tanzania bara hatimaye nyota wa sasa wa timu ya yanga ya tanzania Mrisho Ngassa amewapasha simba.

Nyota huyo aliyasema maneno hayo baada ya kumaliza malipo yote aliyodaiwa kulipa katika ofisi za TFF kwamba fedha sio kitu ila utu ndiyo kitu cha maana hapa duniani

“Mpira ni mchezo wa furaha, hela (fedha) si kitu, kikubwa ni utu, mradi utu wangu mimi hawajauona na nimeisaidia Simba kwa kiasi kikubwa, poa, lakini pamoja na yote sina bifu nao. Ila isipokuwa michezo ni furaha, na mimi nachukulia hii kama changamoto tu,”alisema Ngassa.
Akizungumzia kusimama kwake kucheza mashindano akitumikia adhabu yake hiyo, Ngassa alisema haijamuathiri na zaidi imempa muda zaidi wa kupumzika baada ya kumaliza msimu uliopita.
“Kiwango kushuka au kutoshuka ni mtu mwenyewe jinsi unavyojitunza wakati ambao hauchezi, na kwa ujumla jinsi ambavyo unavyojiweka kisaikolojia, mimi niko sawa na zaidi kupumzika kwa muda fulani, inanipa nguvu ya kurudi na moto zaidi,”alisema.
Kuhusu mlipaji wa deni hilo, kama ni yeye au Yanga, Ngassa amesema; “Katika suala la fedha, nimelipa mwenyewe, kwa hiyo kama kuna mwanachama ambaye ameguswa, anaweza kunisaidia kupoza machungu, lakini sio kama uongozi ndio uliotoa, ni mimi mwenyewe fedha zangu ndiyo nimetoa,”amesema.
Alipoulizwa ni fundisho gani alilolipata baada ya tukio zima hilo, Ngassa amesema; “Nawashauri wachezaji wenzangu kwamba, wanapoingia mikataba na klabu, wahakikishe wanakuwa na mawakili, ili wawasaidie kujua kilichomo ndani yake na wasaini mikataba ambayo wanaielewa,”. 
“Kilichotokea kwangu, kwa Simba ni wamefoji tu, lakini mimi sina bifu nao wala nini, kwa sababu mpira ni mchezo wa furaha, hela si kitu, kikubwa ni utu,”alisema.
Akizungumzia kurejea kwake kazini baada ya kukosa mwanzo wa msimu, Ngassa alisema. “Narudi kuisaidia timu yangu, nina imani itarudi katika nafasi yake,”.
Pamoja na hayo, Ngassa amekiri ushindani mkubwa wa namba uliopo ndani ya Yanga kwa sasa kutokana na timu kusheheni wachezaji wengi bora.
“Changamoto ni kubwa, na kila mchezaji ana uwezo wa kucheza, kikubwa kila mtu akicheza akifanya vizuri, timu inashinda, hilo ndilo kubwa. Nikicheza mimi nikafunga, siyo kama mimi ndiyo nimeshinda, bali ni timu ndiyo imeshinda, hivyo hivyo kwa yeyote akifunga, imeshinda timu,”alisema.
Sakata la Ngassa linaanzia Agosti mwaka jana alipoukera uongozi wa iliyokuwa klabu yake, Azam FC kwa kwenda kubusu jezi ya Yanga SC baada ya kufunga bao la ushindi katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya DRC, Uwanja wa Taifa.
Baada ya kuiwezesha Azam, kutinga fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa 2-1, uongozi ulimuamuru kocha Stewart Hall asimpange mchezaji huyo kwenye fainali dhidi ya Yanga SC, lakini akakaidi na kumpanga na timu ikafungwa.
Kilichofuatia, Azam FC iliamua kutangaza kumuuza mchezaji huyo kwa mkopo na Simba SC wakashinda tenda hiyo, wakati Stewart alifukuzwa na kwenda Sofapaka ya Kenya. Mserbia, Boris Bunjak aliajiriwa Azam, lakini hata kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu uliopita akafukuzwa na Stewart akarejeshwa kazini.
Ngassa aligoma kuuzwa bila idhini yake, lakini Simba SC wakaketi naye mezani na kufikia makubaliano, kabla ya kumtangaza rasmi kujiunga na klabu hiyo. Baadaye Simba SC ikasema ilimuongezea Mkataba mchezaji huyo na kumpa Sh. Milioni 30, wakati yeye mwenyewe anasema alipewa fedha hizo, ili akubali kucheza kwa mkopo.
Yanga SC wakaamini maneno ya Ngassa na alipomaliza muda wake wa kuitumikia Simba SC kwa mkopo kumalizia Mkataba wake na Azam, akasaini kurejea Jangwani.
Hata hivyo, TFF ikabaini mchezaji huyo alisaini Simba SC pia hivyo kumfungia mechi sita na kumtaka arejeshe Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15.     
Ngassa alijiunga na Yanga SC kwa mara ya kwanza mwaka 2007 akitokea Kagera Sugar ya Bukoba na baada ya misimu mitatu akahamia Azam FC, ambako mwaka jana alivuruga na kuuzwa kwa mkopo Simba, kabla ya kurejea rasmi Jangwani, miezi mitatu iliyopita.
Ngassa sasa anatarajiwa kuanza kuichezea Yanga SC kesho katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.





WENGER AJIANDAA KUSAINI MKATABA MPYA NA ARSEAL

Kocha mfaransa  anayefundiaha timu ya arsenal kwa muda mrefu ArsenE wenger anatarajiwa kuongeza au kusaini mkataba mpya na timu hiyo hivi karibuni.

Mfaransa huyo mwenye miaka 63 sasa anatarajiwa kuongeza mkataba utakaomfanyisha akae klabuni hapo kwa muda mrefu.


Awali kocha huyo alitangaza kutoongeza mkataba na timu hiyo na hata kufuatia tetesi za kuhamia timu ya real madrid ya hiapania ili kuifundisha,


Lakini kutokana na supoti kubwa kutoka kwa mmiliki wa timu hiyo Stan Kroenke sasa wenger anatarajiwa kuongeza mkataba wa kuwepo zaidi klabuni hapo.

Wenger na arsenal wana mkataba ambao utaishia msimu huu na ndio maana mmiliki wa timu hiyo anatarajia kukaa na wenger ili kuzungumza kuhusianan na kuongeza mkataba wa kuifundisha timu hiyo ambayo kwa sasa imeanza vizuri katika kampeni zake za kutaka kunyakuwa ubingwa wa uingereza.

HATIMAYE YANGA YAMALIZANA NA NSAJIGWA NA MWASIKA ZAIDI YA MILLIONI 15

Baada ya vuta ni kuvute huku ikitishiwa kulimwa adhabu na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), klabu Yanga imekubali matokeo na kumalizana na wachezaji wake wa zamani, Stephano Mwasika na Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ waliokuwa wakiidai klabu hiyo zaidi ya Sh15 Milioni.
Wachezaji hao walikuwa wanaidai Yanga fedha hizo kutokana na malimbikizo ya ada ya usajili, ambapo uongozi wa klabu hiyo ulikuwa ukiwapiga danadana kuwalipa wakati walipokuwa waikiitumikia.
Kutokana na hali hiyo wachezaji hao baada ya kuachwa na klabu hiyo katika usajili wake wa msimu huu waliamua kuishtaki Yanga ili iweze kuishinikiza na kuwalipa haki zao.
Nsajigwa, alikuwa akiidai Yanga kiasi cha Sh 9 milioni wakati Mwasika ambaye sasa anaitumika Ruvu Shooting alikuwa akiidai Yanga Sh 6.5 milioni.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameliambia gazeti hili jana kuwa wamemalizana na wachezaji hao siku tatu zilizopita.
Alisema Yanga haikuwa na nia ya kuwadhulumu wachezaji hao isipokuwa malipo yao yalichelewa kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali za kiutawala.
“Tumemalizana nao, lakini ni vema ukawauliza na wenyewe kwa uhakika zaidi,” alisema Mwalusako.
Hata hivyo Nsajigwa alipouliwa alikubali kuwa tayari wamemalizana na klabu hiyo tangu siku ya Jumatatu na sasa hana kitu chochote anachoidai klabu hiyo.

DAVID MOYES AMTABIRIA MAKUBWA KAGAWA KATIKA KIKOSI CHAKE, NI BAADA YA KUCHEZA VIZURI DHIDI YA LIVERPOOL JAMATANO

Baada ya kuanzishwa katika kikosi cha kwanza dhidi ya liverpool nota wa kimataifa wa Japan Shinji Kagawa ametabiriwa makubwa zaidi katika kikosi cha manchester united.

Hayo yamekuja baada ya kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya liverpol na kocha wa timu hiyo David Moyes amesema kwamba mchezaji huyo atafanya vizuri zaidi na kumuomba ajaribu kufanya vizuei kila mara anaweza kupata nafasi katika kikos cha kwanza cha timu hiyo.

Washabiki wengi wa soka hususan mashabiki wa manchester united wanaomba mchezaji huyo ajumuishwe kwenye kikosi cha kwanza kwani ana uwezo mkubwa kuliko vaadhi ya wachezaji wanaopangwa katika kikosi hicho.

Wameongeza kwa kusema kiungo huyo anakila kitu ambacho timu hiyo inahitaji kwa muda wote..

VAN GINKEL NJE MIEZI SITA BAADA YA KUUMIA DHIDI YA SWNDON

Kiungo mpya aliyesajiliwa mwaka huu Marco Van Ginkel ameumia na majeruhi yake yatamfanyisha akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa uholanzi aliiumia katika mechi iliyochezwa usiku wa jumanne katika kombe la capital one dhidi ya swindon town baada ya kugongana na Alex Pritchard katikadakika za mwisho za mchezo huo.
 Marco Van Ginkel baada ya kuumia.

Van Ginkel alijiunga na chelsea akitokea vitesse na hatarajiwi kurudi kabla ya April mwakani na ilikuwa mechi yake ya pili kuanza katika kikosi hicho kinacho nolewa na mreno Jose Mourinho.

Thursday, September 26, 2013

YANGA YAMSIKILIZA NGASSA KUHUSIANA NA MALIPO YA MAMILIONI YA SIMBA

Baada ya kumaliza kifungo cha kutocheza mechi 6 za ligi kuu ya vodacom Tanzania bara wiga machachari mrisho ngassa asuburiwa kulipa fedha kwa timu ya simba ilikupewa ruhsa ya kuitumikia tanga katika mchezo ujao wa ligi.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa viongozi wa secretarieti ya timu hiyo mkenya Patrik Naggi
amesema kwamba wanamsikiliza mchezaji huyo kwa malipo hayo na kama akishindwa timu yake ipo tayari kumsaidia kulipa kiasi hicho cha fedha, ili aweze kuitumikia timu yake hiyo katika michezo ya ligi kuu itakayoendelea mwishoni mwa wiki hii.

SIMBA YAJITOA KUWASILI KWA OKWI DAR NA KUSEMA KWAMBA HAWAHUSIKI NA KUJAKWAKE

Klabu ya simba ya tanzania imejitoa kuwasili kwa mshambuliaji wao wa zamani wa timu hiyo waliomuuza huko Tunisia katika timu ya etoel club dusaele Emmanuel Okwi na kusema kwamba hawahusiani na ujuo huo na hawana taarifa zozote.

Hayo yamekuja baada ya watu wengi wakizungumzia ujio wake ni kurudi katika timu hiyo kwa mara nyingine

.Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo msemaji mkuu wa timu hiyo ndugu Ezekiel Kamwaga alisema kwamba hakuna kingozi wa aina yeyote wa simba ambaye yuko karibu na ujio wa nyita huyo kutoka uganda

Vilevile Kamwaga alisisitiza kuwa watu waache kuvumisha habari za kwamba inasemekana simba imemrudisha nyota huyo na kuvunja mkataba na timu yake ktoka tunisia na kuja kujiunga na simba kwa mara nyingine.

Tena aliongeza ni kesi kubwa kuongea na mchezaji wa timu fulani aiwa bado anamkataba wa zaidi  ya miezi sita ili kumsajili.kwa hiyo okwi inawezekana amekuja dar es salaam  ni kwa kazi zake tu na sio kuja kwa ajili ya kujiunga na simba kani bado mchezaji huyo anamkataba na timu yake.

Hata hivyo simba bado wanawadai etoele dusahel dola 30000 ambazo bado simba hawajalipwa kutokana na usajili wa nyota huyo na simba walitarajiwa walipwe mwisho wa mwezi huu.

KUTOKANA NA USHINDI WA JANA DHIDI YA LIVERPOOL MOYES ASEMA KIKOSI KINAANZA KUKAMILIKA

Baada ya ushindi dhidi ya mahasimu wao liverpool kocha wa manchester united david moyes amesema sasa kikosi chake kinaanza kuimarika.

Hayo aliyasema baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari baada ya kumalizika mechi yao ilyopigwa katika uwanja wa old trafford na the red devls kushinda bao moja kwa bila bao lililofungwa na chicharito.

Alisema kwamba anafurahi kuiona timu ikicheza kwa juhudi zote ili kushinda mchezo.Vilevile aliwasifu wachezaji wake kwa ushindi huo kuitia kaptain wa mchezo huo rooney kwani wote walicheza kwa juhudi zote kuhakikisha ushindi unapatikana.

Kocha huyo raia wa scotland ameendelea kwa kuwaomba mashabiki wa timu hiyo kuisupport pind iwapo uwanjani na kuwa na matumaini na timu yao kila mara ili kuwaweka wachezaji katika hali ya kujiamini zaidi kwa kila mchezo japokuwa timu ipo katika kipindi cha mpito.

KUTOKANA NA KIPIGO CHA MAN CITY JUMAPILI ILIYOPITA MOYES AIMBIA JAMII YA SOKA KWAMBA KINAWEZA KURUDIA TENA KWANI TIMU IPO KWENYE KIPINDI CHA MPITO

Kocha wa Manchester United David Moyes amewaonya mashabiki wa mabingwa wa ligi kuu ya England kwamba anahitaji kuimarisha kikosi chake na kwamba kipigo cha Jumapili ambapo walichapwa 4-1 na Manchester City huenda isiwe ndio mwisho wa matokeo kama hayo.
"Kutatokea siku kama ile ya Jumapili na huenda tukakabiliwa na matokeo zaidi kama hayo kwa sababu tuko katika kipindi cha mpito," aliwaaambia waandishi habari kabla ya pambano la Jumaatano la kombe la Capital One dhidi ya Liverpool.

"Tulihitaji wachezaji wawili watatu hivi ambao wangeweza kuingia moja kwa moja katika timu. Lakini hayo yatatokea, kweli huenda itabidi nikabiliane na vipigo vichache zaidi. Bado tunakabiliwa na kazi pevu ya kuwasajili wachezaji sio tu watakaojumuishwa na kikosi chetu lakini wenye uwezo wa kuingia moja kwa moja katika timu," aliongeza kusema Moyes katika msimu wake wa kwanza katyika a Old Trafford baada ya kushikikilia nafasi iliyoachwa na Alex Ferguson.
Manchester United iliwakosa wachezaji kadhaa mastaa wakati wa kipindi kilichopita cha usajili na hata kulikua na tetesi za juhudi za dakika ya mwisho za kuipiku Real Madrid ili kumsajili Gareth Bale ambae kuuzwa kwake kutoka Tottenham Hotspur kulivunja rekodi kama mchezaji ghali kupita wote duniani.
Juhudi za kuwasajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona, Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao na Fabio Coentrao kutoka Real Madrid ziliambulia patupu.
Leighton Baines aliamua kubaki Everton wakati Thiago Alcantara aliamua kuihama Barcelona na kujiunga na Bayern Munich.
Moyes badala yake alikimbilia kumsajili mchezaji wa kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini, kutoka klabu yake ya zamani Everton, kwa dola millioni ($43.96 ) dakika chache tu kabla ya kufungwa dirisha la usajili.

VIDEO: CHICHARITO AKIIUA LIVERPOOL

VIDEO:RONALDO AKIPIGA MBILI DHIDI YA ELCHE

CHICHARITO AITOA LIVERPOOL KWENYE CAPITAL ONE LIGUE

 chicharito akiifungia goli manchester united.

Mmexico javer hernandez "chichariti" jana usiku ilichukuwa dakika ya 46 ni muda mchache tu baada ya kipindi cha pili kuanza kuipatia timu yake ya manchester united goli kupitia kona iliyochongwa maridadi na rooney.
 chicharito akishangilia goli.

Katika mchezo huo kocha wa manchester alianzisha kikosi cha vijana huku akimjumuisha mkongwe giggs. Safu ya ulinzi ilikuwa inaongozwa na smalling na evans, rafael na buttner. Kwenye kiungo kulikuwa na jones ,giggs ,kagawa, nani huku safu ya ushambuliaji ilikuwa na kaptain wa mchezo wa jana wyne rooney na chicharito.
Phil jones akifanya vitu vyake katikati akimzuia suarez
Rooney akiachia shuti lililookolewa na mignoilet dakika ya 84

RONALDO APIGA MBILI HUKU MADRID IKIINYUKA ELCHE 2-1

Katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu ya hispania zilizochezwa jana usiku timu ya real madrid yainyuka timu ya Eiche kwa mabao 2-1.

Ilichukuwa dakika nyingi kwa madrid kuapata bao kwa hadi kipindi cha kwanza kulikuwa hakuna timu iliyopata bao.
 Cristiano ronaldo akifunga bao la pili kwa penalt.

Baada ya kurudi mapumziko madrid walianza kupata bao kupitia kwa nyota wao cristiano ronaldo katika dakika ya 51. Kutokana na mchezo kuwa mali na wakusisimua huku Elche wakicheza kwa kujiamini ndani ya uwanja wao wa Estadio Manuel Martinez Valero walifani kiwa kusawazisha goli hilo dakika ya nyongeza ya 91 kupitia kwa Boakye.
 Gareth bale na wenzake wakishangilia goli lililofungwa nacristiani ronaldo.

Katika mchezo huwo refaree aliongeza dakika sita na katika dakika ya 96 madrid walipata penalt na nyota wao ronaldo kuipatia goli la ushindi.

IBRAHIMOVIC AONGEZA MKATABA PSG

Mshambuliaji wa PSG ya ufaransa na timu ya taifa ya sweden hatimaye ameongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo baada ya tetesi nyingi za usajili dhidi yake kuhamia ligi kuu ya uingereza.

Nyota huyoaliyewahi kuzichezea timu za inter milan, barcelona na ac milan ameoneza mkataba huo utakao mfikisha hadi mwaka 2016.


Wednesday, September 25, 2013

VIDEO: NEYMAR AKIIFUNGIA BARCELONA GOLI LAKE LA KWANZA KATIKA LIGI HUKU BARCA IKISHINDA 4-1 DHIDI YA REAL SOCIEDAD

LEVANDOWSKI: NITASAINI BAYERN JANUARY

Mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya poland na clabu ya borussia dortmund roberto lewandowski amesema kwamba yupo tayari kusaini atika clubu ya bayern munich mnamo january mwakani.

Hii imekuja baada ya dili lake la kwanza katika majira ya joto kufa na anatarajia kujiunga na timu hiyo mnamon january mwakani.

Mchezaji huyo mwenye ndoto kubwa za kuichezea timu hiyo tangu akiwa mdogo amesema kwamba anaipenda sana timu hiyo na yupo tayari kujiunga nao na sio timu yeyote tofauti na bayern munich. 

BOLT KUONGEZA MKATABA NA KAMPUNI YA PUMA

Mwanariadha mashuhuri duniani kutoka Jamaika Usain Bolt anatarajiwa kuongeza mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya puma.

Mfukuza upepo huyo anatarajiwa kuongeza mkataba hadi kipindi kingine cha mbio za duinia. Mkataba huo utakuwa wa kipindi cha miaka miwili.

Usain Bolt ameweka rekodi ya sekunde 9:58 katika mbio za mita 100 na ni mshabiki namba 1 wa manchester united.

BAADA YA KUMALIZA ADHABU YA KUTOCHEZA MECHI 6 NGASSA ATAKIWA KULIPA FAINI ALIYOPEWA KUWA HURU

Winga machachari wa timu ya taifa ya Tanzania taifa stars na timu ya yanga sc Mrisho ngassa hatimaye memaliza adhabu aliyopewa na TFF kutocheza michezo6 ya ligi u ya tanzania bara VPL.

Lakini mchezaji huyo bado hayuko huru kwani bado anatakiwa alipe faini aliopewa ilikuwa huru, na kwa mujibu wa TFF anatakiwa alipe kiasi cha fedha.

Uongozi wa timu ya Yanga unasem bado wanamsikiliza ngassa kuhusiana na malipo ya faini hiyo ili aweze kutumiwa katika michezo ya ligi inayoendelea kwani yuko fiti na anafanya mazoezi na wachezaji wenzake kila siku.

Kwa mujibu wa maneno hayo inaelekea hata uongozi haujui nani atalipa ni yeye mwenyewe au uongozi utafanya maamuzi ya kumlipia. Kwa ushauri tu uongozi mlipieni kijana wenu ili acheze kwani yupo mikononi mwenu.

DI CANIO ATIMULIWA SUNDELAND

Kocha wa timu ya sunderland ya uingereza robato di canio hatimaye ametimuliwa rasmi kuifundisha timu hiyo baada ya matokeo mabovu katika ligi kuu ya uingereza.

Uongozi wa timu hiyo umemtimua kocha huyo mwenye vituko akiwa uwanjani baada ya maneno machafu kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kupigwa mabao3-0 na west bromwich jumamosi iliopita.

Hadi hivi sasa timu hiyo inaburuza mkia kwa kuwa timu ya mwisho katika msimamowa ligi hiyo ilihali uwongozi wa timu hiyo ulimpa fedha za usajili lakini hakuna mabadiliko yeyote.

Kocha huyo hadi anaiaca timu hiyo alikuwa ameshafikisha mechi 13 na kushinda mechi 3 tu. Hata hivyo kocha huyo aliinusurisha timu hiyo kushuka daraja baada ya kuikuta timu hiyo katika wakati mgumu.

Kwa mujibu wa uongozi wa timu hiyo unafanya mchakato wa kumtafuta kocha mpya na hadi sasa wamemfikiri kumleta Robato Dimatteo kurithi mikoba hiyo.

Hizi ni baadhi za picha zinazomuonyesha di canio katika vituko:

TWIGA STARS YAPANGWA NA ZAMBIA

Timi ya taifa ya wanawake ya tanzania imepangwa kucheza na timu ya taifa ya zambia katika mchezo wa kukata tieti kucheza mataifa ya afrika kwa soka la wanawake.

Timu hiyo itaanza kampeni zake mnamo may mwakani na kurudiana july ili kupata tiketi itakayo wapeleka katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Namibia.

Tuesday, September 24, 2013

LUIS SUAREZ KURUDI DHIDI YA MANCHESTER UNITED KESHO KWENYE LEAGUE CUP

Baada ya kifungo cha muda mrefu cha mechi 10 baada ya kumng'ata beki wa chelsea Ivanovic hatimaye luis suarez kurudi kesho dhidi ya manchester united kwenye legue cup

Manchester united watamkaribisha mashambuliaji huyo raia wa Uruguay ambapo itapata wakati mgumu kumzuia pamoja na Daniel Sturridge ambaye yupo on fire.Hata hivyo the red devils nao watajituma ili kufucha aibu walioipata ya kupigwa mabao 4-1 na man city pia liverpool nao watahitaji kushinda kwani nao woki iliopita walipoteza dhidi ya southempton kwa goli 1-0.

Mchezo huwo utakuwa mkali na wa kusisimua kwa kuwa kila timu inatahitaji kushinda ili kuji hakikishia kuendelea na kuligombania kombe hilo na pia kwa man united kulipiza kisasi sha kufungwa na liverpool katika ligi kuu ya uingereza wiki mbili zilozopita.


ROONEY: MECHI KATI YA LIVERPOOL NI KUBWA KULIKO NA MAN CITY

Nota wa kimataifa wa england wyne rooney amebainisha kwamba mechi yao dhidi ya liverpool ni kubwa kuliko na man city.

Hayo aliyasema jana baada ya mazoezi akiulizwa kuhusiana na mchezo huwa atakaofanyika kesho jumatano wa kombe la capital one kwamba, "ni mchezo mgumu na si wakulinganisha dhidi ya man city kwani kila mtu huwa kivingine na hata mimi huwa najisikia tofauti ninapocheza dhidi ya liverpool "

Aliongeza kwa kusema kuwa wanatumaini kushinda ili kujiweka vizuri kisaikolojia kwa michezo ya baadae.

ROBATO DI MATTEO KUMRITHI PAOLO DI CANIO SUNDERLAND

Kocha aliyetwaa kombe la ligi ya mabingwa ulaya  Robato Di Matteo na timu ya chelsea mwaka 2012 huwenda akachukua mikoba ya di canio ndani ya sunderland.

Akizungumza na waandishi wa habari katika press conference kiongozi mkuu wa sunderland amesema kwamba jicho lao la kwanza ni kufikiria kumwambia di matteo kuja kuchukuwa mikoba ya di canio baada ya kuanza vibaya ligi kuu ya uingereza.

Timu hiyo ndio inayoshika nafasi ya mwisho ikiwa imefungwa zote na kutoka sare mchezo mmoja tu na haijshinda hata mchezo mmoja.

Uongozi wa timu hiyo unafikiria kumshawishi kocha huyo mzoefu mwenye historia nzuri na clabu ya chelsea kwa kuwa wakwanza kuipa ubingwa wa mabingwa ulaya tangu ilipoanzishwa timu hiyo licha ya timu hiyo kupitiwa na makocha wakubwa duniani .

VIDEO : FUJO WASHABIKI WAINGIA NDANI YA UWANJA MECHI KATI YA GALATASARAY VS BESIKTAS

VIDEO:MANCHESTER UNITED IKICHAPWA 4-1NA MANCHESTER CITY

Monday, September 23, 2013

BAADA YA KICHAPO CHA MABAO 4-1 KUTOKA KWA MANCHESTER CITY, MSHAMBULIAJI WA MANCHESTER UNITED WYNE ROONEY ANENA....

Kutokana na matokeo mabaya dhidi ya mahasimu wao kutoka jiji moja la manchester, mshambuliaji hatari wa manchester united wyne rooney azungumzia mchezo huo.

Rooney alisema kwamba ulikuwa ni mchezo mgumu kwao tangu dakika 15 za kwanza katika kipindi cha kwanza na walianza kupoteana na kutojua la kufanya zaidi ya kujaribu kuzuia tu ili magoli yasiingie lakini wachezaji walikuwa makini na kuweza kupata goli la kwanza mnamo dakika ya 16.

Baada ya dakika hizo na kupatikana kwa goli la kwanza tukaanza kupoteza kujiamini na kuwaachia wapinzani kumiliki mpira zaidi na sisi kujaribu kuzuia na ndipo safu yetu ya ulinzi kuelemewa zaidi huku kiungo kilikuwa hakina cha kufanya zaidi ya kuokoa tu.

Vilevile rooney alisema kwa kuliomba benchi la ufundi kuimarisha safu ya ulinzi kwani ilikuwa inapoteana kila muda kutokana na kasi ya washambuliaji wa timu pinzani, lakini aliwapongeza wachezaji wenzake kuendelea kujituma hadi dakika za mwisho na kulinda wapinzani wasipate goli lingine baada ya dakika ya 55.

Mwisho alisema cha kufanya ni kusahau na kuangalia yajayo katika mechi yao dhidi ya liverpool jumatano katika kombe la capital one na kuamini kuwa watashinda mchezo huwo japokuwa liverpool itamchezesha mchezaji wake luis suarez kwa mara ya kwanza baada ya kumalia adhabu.

PHOTOS:FUJO MCHEZO WA GARATASARAY VS BESIKTAS KATIKA LIGI KUU YA UTURUKI WASHABIKI WAINGIA NDANI YA UWANJA NA MCHEZO KUVUNJIKA

Mchezo wa ligi kuu ya uturuki uliofanyika jana jumapili uliishia kwa vurugu na washabiki kuingia uwanjani kabla ya mchezo kuisha.

Mechi hiyo hadi inavunjika timu ya garatasaray ilikuwa inaongoza kwa magoli 2-1 huku Drogba akifunga mabao yote kwa upande wa garatasaray akisawazisha na kuongeza ndipo mashabiki wa besiktas kuingia uwanjani na mwamuzi kuvunja mchezo huwo.